Select a Verse

Zaburi 124

Shukrani Kwa Ukombozi Wa Israeli

Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.

1Kama Bwana asingalikuwa upande wetu;

Israeli na aseme sasa:

2kama Bwana asingalikuwa upande wetu,

wakati watu walipotushambulia,

3wakati hasira yao ilipowaka dhidi yetu,

wangalitumeza tungali hai,

4mafuriko yangalitugharikisha,

maji mengi yangalitufunika,

5maji yaendayo kasi

yangalituchukua.

6Bwana asifiwe,

yeye ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao.

7Tumeponyoka kama ndege

kutoka mtego wa mwindaji;

mtego umevunjika,

nasi tukaokoka.

8Msaada wetu ni katika jina la Bwana,

Muumba wa mbingu na dunia.