Select a Verse

Zaburi 129

Maombi Dhidi Ya Adui Za Israeli

Wimbo wa kwenda juu.

1Wamenionea mno tangu ujana wangu;

Israeli na aseme sasa:

2wamenionea mno tangu ujana wangu,

lakini bado hawajanishinda.

3Wakulima wamelima mgongo wangu,

na kufanya mifereji yao mirefu.

4Lakini Bwana ni mwenye haki;

amenifungua toka kamba za waovu.

5Wale wote waichukiao Sayuni

na warudishwe nyuma kwa aibu.

6Wawe kama majani juu ya paa,

ambayo hunyauka kabla hayajakua;

7kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake,

wala akusanyaye kujaza mikono yake.

8Wale wapitao karibu na wasiseme,

“Baraka ya Bwana iwe juu yako;

tunakubariki katika jina la Bwana.”