Select a Verse

Zaburi 134

Wito Wa Kumsifu Mungu

Wimbo wa kwenda juu.

1Msifuni Bwana, ninyi nyote watumishi wa Bwana,

ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Bwana.

2Inueni mikono yenu katika pale patakatifu

na kumsifu Bwana.

3Naye Bwana, Muumba wa mbingu na dunia,

awabariki kutoka Sayuni.